MFALIME wa taarab hapa nchini, Mzee Yussuf kutoka kundi la Jahazi Modern Taarab atakuwa miongoni mwa wasanii watakaoporomosha burudani katika shindano la kumsaka mrembo wa Kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014).
Shindalo hilo litafanyika siku ya sikukuu ya Nanenane kwanue ukumbi wa Nashera Hotel, mkoani Morogoro.
Miss Kanda ya Mashariki itashirikisha jumla ya warembo 14 kutoka mikoa minne ya Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro na itakuwa chini ya udhamini wa Redds Original, Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari Lodge, Kitwe General Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC Africa, Sykes Travel, Sasa Saloon, Grand Villa Hotel, Shabibi Line na Clouds FM.
Mratibu wa masindano hayo, Alex Nikitas aliwataja warembo watakaoshindana siku hiyo kuwa ni Lucy Julius Diu, Prisca Mengi, Tarchisia Noback Mtui na Angel Shio ambao wanatoka Morogoro.
Warembo wengine ni Elizabeth Tarimo, Lilian Andrew na Leila Abdul Ally ambao wanatoka mkoa wa Lindi ambapo kutoka Mtwara ni Nidah Fred Katunzi, Lightness Mziray na Nelabo Emmanuel.
Pia warembo kutoka Pwani ni Khadija Ramadhan Sihaba, Irene Rajabu Soka, Mary Mpelo na Arafa Shaban. Nikitas alisema kuwa warembo hao watakuwa kambini kuanzia Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge chini ya ukufunzi wake Miss Kanda ya mashariki wa mwaka jana, Diana Laizer.
Comments
Post a Comment