MIKAEL SILVESTRE APONDA USAJILI WA ALEXIS SANCHEZ ARSENAL …adai si aina ya mchezaji anayehitajika Emirates



MIKAEL SILVESTRE APONDA USAJILI WA ALEXIS SANCHEZ ARSENAL …adai si aina ya mchezaji anayehitajika Emirates

Arsenal, Alexis Sanchez, Transfer News

MCHEZAJI wa zamani wa Arsenal Mikael Silvestre amesema Arsene Wenger alistahili kusajili mshambuliaji aina ya Olivier Giroud badala kutumia pauni milioni 35 kwa ujio wa Alexis Sanchez.

Beki huyo ambaye alikuwa na misimu miwili isiyo na mafanikio Emirates akitokea Manchester United mwaka 2010,  anaamini nyota huyo wa Chile katika kombe la dunia si aina ya mchezaji aliyestahili kununuliwa na klabu hiyo.

Silvestre, 36 anasema kwamba licha ya Sanchez kuchukuliwa kama mmoja wa washambuliaji bora duniani, hakustahili kwenda Emirates katika kipindi hiki ambacho Arsene Wenger ana wachezaji wengi wa aina hiyo kwenye kikosi chake. "Alistahili kununua 'muuaji' kama Olivier Giroud," anaeleza beki huyo aliyepata pia kuwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa.

"Sanchez angeweza kwenda kokote pale baada ya kung'ara kwenye michuano ya kombe la dunia lakini sidhani ni mchezaji anayehitajika Arsenal kwa sasa," aliongeza.

Maoni hayo ya Silvestre yanatarajiwa kuwachukiza mashabiki wa Arsenal ambao walifurahia sana kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona.



Comments