MIDO KITUMBUA CHAINGIA MCHANGA ZAMALEK




MIDO KITUMBUA CHAINGIA MCHANGA ZAMALEK
NA FULLSHANGWE
MAISHA ya soka ya Mido yameingia ukurasa mwingine baada ya kufukuzwa kazi ya ukocha mkuu na klabu yake ya Zamalek jana jumanne.
Kocha huyo kijana mwenye miaka 31 aliripotiwa kuwa na mgogoro na bodi ya klabu na kusababisha kibarua chake kuota nyasi, japokuwa inasemekana kuwa ataendelea kuwa sehemu ya miamba hiyo kwa majukumu mengine.
Mido alirithi mikoba ya Helmy Toulan mwezi januari mwaka huu na aliiongoza timu hiyo kucheza mechi za mwisho za ligi ya ndani na kutwaa ubingwa wa kombe la Misri mbele ya klabu ya Smouha.
Licha ya kupata mafanikio hayo, Mido aliyekaa kwa miezi saba tu aliripotiwa kuwa na matatizo mengi na bodi ya klabu hiyo, lakini mshambuliaji huyo wa zamani wa Zamalek atapewa majukumu mengine klabuni hapo.
Mido alisema: "Ahmed Suliman kutoka bodi ya ukurugenzi ameniambia maamuzi yao ya kunifukuza".
"Bado ni mtoto wa Zamalek na niko tayari kufanya kazi yoyote kuisaidia klabu".

Mido alistaafu kucheza soka akiwa na miaka 30 mwezio juni mwaka 2013, huku akiwa amezichezea klabu 12 tofauti, zikiwemo Zamalek, Ajax, Marseille, Roma na Tottenham, kabla ya kuichezea Barnsley alipotundika daruga zake.


Comments