Muda mfupi baada ya   kujiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 63, mchezaji wa   Colombia James Rodriguez ameweka rekodi katika mauzo ya jezi yake ya Real   Madrid.Ripoti za Hispania zinasema Jezi zipatazo 900 za James Rodriguez ziliuzwa   ndani ya saa moja tangu zilipoingia rasmi sokoni ambapo zimeuzwa kwenye duka la   Real Madrid na imeonyesha kiasi gani raia huyu wa Colombia   anavyokubalika.
Rodriguez ametua   Madrid akitokea AS Monaco huku akiwa ndiye mfungaji bora wa Kombe la Dunia   nchini Brazil 2014 baada ya kutokana na magoli 6   aliyofunga.
Comments
Post a Comment