MASHUJAA BAND MATAWI YA JUU, PATA PICHA 8 ZA MAMAA SAKINA NA CHAZ BABA WAKITIMKIA AFRIKA KUSINI …wanakwenda kuboresha albam ya Ushamba Mzigo, kumnyakua msanii wa South

MKURUGENZI wa Mashujaa Band,  Sakina Mbange "Mamaa Sakina" na Rais wa bendi Chaz Baba mchana huu wameruka kuelekea nchini Afrika Kusini kwaajili ya kufanya mambo kadhaa ya maendeleo ya bendi.

Viongozi hao wa Mashujaa wameondoka kwa ndege ya shirika la South African Airways na watakaa huko kwa siku moja kabla ya kurejea Jumapili kabla ya kuanza ziara yao ndefu ya mikoani.

Akiongea na Saluti5 kabla ya kupaa hewani, Chaz Baba alisema wanakwenda kufanya mastering ya albam yao ya "Ushamba Mzigo" ikiwa ni pamoja na kufanya makubaliano na moja ya makampuni ya huko ili kuchapisha nakala za audio CD ya albam hiyo tayari kwa kuingia rasmi sokoni.

"Tunakwenda kuboresha albam yetu ya "Ushamba Mzigo" lakini pia tunatarajia kufanya maongezi na msanii mmoja anayefanya kazi Afrika Kusini kwaajili ya kujiunga na Mashujaa Band", alisema Chaz Baba.

Albam ya "Ushamba Mzigo" ndio albam bora ya mwaka kwa mujibu wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards.

Mamaa Sakina (kushoto) akiwa na Chaz Baba uwanja wa ndege wa kimataifa Dar es Salaam
Mamaa Sakina (kushoto) akiwa na Chaz Baba
Mamaa Sakina (kulia) akiwa na Chaz Baba ndani ya ndege tayari kwa safari
Chaz Baba ndani ya ndege
Mamaa Sakina  na Chaz Baba ndani ya ndege 
Mamaa Sakina  na Chaz Baba
 Mamaa Sakina 
Chaz Baba

Comments