MASHUJAA BAND KUIZUNGUKA TANZANIA NZIMA …kutia mguu hadi KENYA …uhondo unaanzia Mtwara Idd Mosi …Bavaria yatoa udhamini
BENDI bora ya dansi kwa mwa mwaka wa pili mfululizo, Mashujaa Band inatarajia kufanya ziara kubwa ya kuzunguka karibu mikoa yote ya Tanzania, hii ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya bendi hiyo.
Ziara hiyo itakayochukua zaidi ya wiki mbili, ambayo itahusika hadi maonyesho kadhaa nchini Kenya, inakuja kufuatia maombi mengi ya mashabiki wa mikoani lakini pia ni pamoja na kutoa shukran kwa wapenzi wao kila sehemu walioiwezesha Mashujaa Band kutwaa tuzo tatu za Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Kwa mujibu wa ratiba ambayo Saluti5 imetumiwa na Mkurugenzi Masoko wa Mashujaa, Max Luhanga, ni kwamba ziara hiyo itaanzia Mtwara siku ya Idd Mosi katika ukumbi wa Makonde Beach huku Idd Pili wakiwa Masasi katika ukumbi wa kisasa wa Emirates.
Katika hali ya kuvutia zaidi, Saluti5 imeambiwa kuwa zaidi ya nusu ya show hizo tayari zimenunuliwa na mapromota wa mikoani hali inayoonyesha ni namna gani watu wana hamasa na ziara hiyo ya Mashujaa Band.
Kinywaji cha Bavaria kimedhamini ziara hiyo ya Mashujaa na tayari magari mawili (mini bus na gari la vyombo) yameshapigwa chata za kuvutia kunadai tripu hiyo. Mwishoni mwa habari hii utapata picha 6 za magari hayo.
Ratiba kamili ya ziara hiyo ya Mashujaa Band ni kama ifuatavyo.
IDD MOSI: MAKONDE BEACH- MTWARA.
IDD PILI: EMIRATE HALL- MASASI
30-07-2014 NACHINGWEA- NACHINGWEA RESORT
31-07-2014 MBINGA-MBINGA RESORT
01-08 2014 SONGEA-SERENGETI PUB
02-08-2014 MBEYA-CITY PUB
03-08-2014 MBALALI TOP LIFE
05-08-2014 TUNDUMA-HIGH CLASS
06-08-2014 SUMBAWANGA-MWAMBAO PUB
07-08-2014 MPANDA- KATAVI RESORT
08-08-2014 KIGOMA-SANDRA NIGHT CLUB
09-08-2014 TABORA- BWALO LA MAOFISA WA POLISI.
10-08-2014 SHINYANGA-NSSF HALL
13-08-2014 KAHAMA- CLUB CHILLER
14-08-2014 BUKOBA- LINAS CLUB
15-08-2014 GEITA-DESIRE CLUB
16-08-2014 MWANZA-VILLA PARK
17-08-2014 MWANZA-BUZURUGA
20-08-2014 MUSOMA MAGEREZA HALL
21-08-2013--KENYA 22-08-2014--KENYA 23-08-2014--KENYA 24-08-2014--KENYA
28-08-2014 KOROGWE MAMBA CLUB
29-08-2014 TANGA - NYUMBANI HOTEL
30-08-2014 ARUSHA - TRIPPLE A
31-08-2014 SINGIDA - LAKE GARDEN
05-09-2014 DODOMA- CANIVALL
06-09-2014 Dar...Kill Award Event.
07-09-2014 MOROGORO-NYUMBANI PARK.
Max Luhanga amesema maonyesho mengine ya mikoani yanaweza kuongezeka kadri ya mahitaji ya mapromota wa sehemu husika.
Pichani ni namna magari ya Mashujaa Band yalivyoandaliwa kwa ziara hiyo.
Comments
Post a Comment