MAPACHA WATATU KULA IDD MOSI BAGAMOYO …AKUDO IMPACT MSASANI BEACH KAWE


MAPACHA WATATU KULA IDD MOSI BAGAMOYO …AKUDO IMPACT MSASANI BEACH KAWE
MAPACHA WATATU KULA IDD MOSI BAGAMOYO …AKUDO IMPACT            MSASANI BEACH KAWE

BENDI ya Mapacha Watatu leo Idd Mosi watatumbuiza kwenye tamasha kubwa la Idd litakalofanyika Chuo cha Sanaa mjini Bagamoyo.

Katika Tamasha hilo Mapacha Watatu wataungana  na wasanii wengine kama Snura Mushi, Kingwendu, Msaga Sumu, Babu Ayuob, Onyango na Mwita Maranya.

Waandaji wa onyesho hilo, Media Assistant, wameiambia Saluti5 kuwa tamasha hilo litakaloanza mchana hadi usiku wa manane, litatumbuizwa pia na kundi la taarab la Super Shine Modern Taarab.

Wakati huo  huo bendi ya Akudo Impact itafanya bonanza kubwa la Idd ndani ya ukumbi wao wa nyumbani Msasani Beach Club Kawe jijini Dar es Salaam.

Rais wa Akudo Impact Tarsis Masela ameiambia Saluti5 kuwa watatumia onyesho hilo kama fursa ya kutambulisha nyimbo zao mpya kabisa.



Comments