Najua headlines za   huyu mkali wa soka mwenye asili ya Kenya anaeichezea timu ya taifa ya Ubelgiji   kujiunga na Liverpool sio mpya kwa wafatiliaji wa soka lakini sasa baba yake   mzazi ameongea na reporter  Julius Kepkoech.
  Mike Origi Okoth   amedokeza kwamba kuna timu nyingine ambayo hajaitaja lakini inamtaka   mshambuliaji huyu kama zilivyo Liverpool na Tottenham ambapo pamoja na hayo,   amesisitiza kwamba hatma ya Divock ni sharti iamuliwe ifikapo Jumatatu wiki   ijayo japo Divock mwenyewe bado hajafanya uamuzi kuhusu uhamisho wake japo   Liverpool inabaki kuwa timu yenye nafasi kubwa ya kumsajili   Divock.
Comments
Post a Comment