MANCHESTER UNITED YAOKOTA USHINDI WAKE WA PILI, YAICHAPA AS ROMA 3-2…Rooney kama kawa, Roma waiteka show kwa bao la ajabu
MANCHESTER United imeendelea kutakata kwenye mechi zake za majaribio baada ya kuinyuka AS Roma ya Italia kwa bao 3-2.
Huu unakuwa mwanzo mzuri kwa kocha Louis van Gaal ambaye majuzi alishuhudia kikosi chake kikiangusha kipigo cha maangamizi 7-0 kwa LA Galaxy.
Kama ilivyokuwa mechi ya kwanza, Rooney ameng'ara tena kwa kutupia wavuni mabao mawili, moja kwa mkwaju wa mita 25 kunako dakika ya 36 na lingine kwa penalti dakika ya 44.
Juan Mata naye aliifungia United kwa bao lake maridadi dakika ya 39.
Hadi mapumziko, United ilikuwa mbele 3-0 lakini ikajikuta ikibanwa kipindi cha pili na kuruhusu mabao mawili.
Lilikuwa ni bao la kwanza la Roma kupitia kwa Pjanic dakika ya 75, ndilo lililoteka simulizi za mchezo huo kufuatia shuti lake la mita 60 kwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa Amos akiruka bila mafanikio. Totti akaifungia Roma goli la pili kwa njia ya penalti dakika ya 88.
Manchester United: (3-5-2) Johnstone 5.5 (Amos 45mins 6); Blackett 5.5, Jones 6 (M Keane 45mins 6), Evans 6 (Smalling 45mins 6); Valencia 5.5 (Young 45mins 5.5), Herrera 6 (Nani 45mins 5), Cleverley 5 (Hernandez 69mins 6), Mata 7 (Kagawa 45mins 6), James 6 (Shaw 45mins 6.5); Rooney 8.5 (W Keane 45mins 6), Welbeck 6.5 (Lingard 45mins 6)
AS Roma: (4-2-3-1) Skorupski; Calabresi (Somma 45mins), Benatia, Romangnoli (Castan 45mins), Emanuelson (Cole 45 mins); Ucan, Keita (Pjanic 68mins 7.5); Iturbe (Ljajic 45mins), Paredes (Nainggolan 45mins); Florenzi (Totti 68mins); Destro
Comments
Post a Comment