Paul                Scholes (kushoto) alikuwepo katika mechi ya jumanne wakati                 Salford City  inacheza dhidi ya Stalybridge Celtic, klabu                ambayo ana hisa, ikiwa ni mechi ya maandalizi ya kabla ya                msimu.
          MANCHESTER                United wamemuambia kiungo wake wa zamani Paul Scholes kuwa                milango ipo wazi kwake kurudi kufanya kazi ya ukocha Old                Trafford.
          Scholes                alikuwa sehemi ya benchi la Ryan Giggs wakati                alipokabidhiwa timu kwa muda mwishoni mwa msimu wa mwaka                jana kufuatia kufukuzwa kazi kwa kocha mkuu David Moyes.Giggs aliingoza Man United katika mechi              nne za mwisho za ligi kuu soka nchini England.
                    Watu                walidhani Scholes ameamua kuitosa Man United majira ya                kiangazi baada ya kuwakosoa vikali baadhi ya wachezaji wa                timu hiyo kwenye fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
          Scholes                aliuliza kama tayari Wayne Roonye amepita miaka yake  28                ya ubora na aliuliza kwanini klabu imemsajili Luke Shaw                kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 30.
           Inafahamika                kuwa kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal na                mkurugenzi mkuu Ed Woodward bado wanaamini  kiungo huyo                nyota wa zamani wa England ana kitu cha kuisaida klabu.
          Scholes                ameambiwa kuwa klabu itafurahi kama watafanya mazungumzo.
          Lakini                hatapewa kazi katika timu ya kwanza kutokana na Van Gaal                kuridhishwa na wasaidizi wake wa sasa.
         Scholes                alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Ryan Giggs mwishoni                mwa msimu wa mwaka jana.
          Hata                hivyo, United wanataka kumpa kazi Scholes ya kufundisha                kikosi cha vijana ili asaidiane na kocha wa sasa Nicky                Butt.
          "Bado                tunatambua thamani na ubora wa juu wa Scholes". Chanzo                kutoka United kilisema.
          "Milango                ipo wazi kwake kurudi".
        
Comments
Post a Comment