Haris Fetahović, Daniel Bigas                Alsina, Dino Julardžija
        PRESS RELEASE
        SABMiller
        Dar es Salaam, Tanzania, July 31, 2014
        Imechapishwa Julai 31, 2014, saa                3:16 asubuhi
        Makocha wa FC Barcelona wawasili kutoa              mafunzo kwa makocha wa Tanzania
        CASTLE Lager, bia inayoongoza barani              Afrika na FC Barcelona, moja kati ya timu kubwa zaidi za              soka duniani wameshirikiana kuleta makocha kutoka klabu hiyo              yenye makao yake huko Camp Nou, Hispania ili kutoa mafunzo              ya mbinu za soka kwa makocha wa Tanzania wiki hii. Makocha              hao wa FC Barcelona ambao wataendesha mafunzo hayo wamefika              jijini Dar es salaam leo (31/8/2014).
        Mafunzo hayo yatafanyika kwenye uwanja wa              Karume jijini Dar es salaam kwa siku mbili zijazo ambazo ni              tarehe 1 na tarehe 2 Agosti na yataendeshwa na makocha              waliobobea kwenye mbinu mbalimbali za kandanda ikiwemo Tiki              Taka.
         Makocha hawa ni Daniel Bigas Alsina and              Isaac Oriol Guerrero Hernandez kutoka Shule ya Soka ya FB              Barcelona.
        Mafunzo haya ni sehemu ya manufaa ya              ushirikiano uliosainiwa mwaka jana kati ya FC Barcelona na              Castle Lager ambayo ni bia rasmi ya FC Barcelona barani              Afrika. Vilevile, mafunzo haya ni sehemu ya manufaa ya              ushirikiano huu kwa jamii.
        Kupitia mafunzo haya, makocha 30              waliobahatika kutoka ligi kuu na ligi daraja la kwanza              watapata fursa maalum ya kujifunza mbinu mbalimbali za              mazoezi zinazotumiwa na FC Barcelona na kufanikiwa              kuwatengeneza baadhi ya wachezaji wenye mafanikio makubwa              zaidi duniani."Tuna shauku kubwa sana kuona              mafunzo haya yanakuja Tanzania na tunafurahia kupata nafasi              ya kurudisha fadhila kwa jamii ambayo inatuunga mkono.              Tunaamini mafunzo haya yatawanufaisha makocha na wachezaji              wa Tanzania katika siku zijazo," alisema Fimbo Buttallah,              Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania.
        "Castle Lager ina historia kubwa na soka              barani Afrika na tukio hili litazidi kuimarisha uhusiano              uliopo kati ya bia namba moja Afrika na mchezo namba moja              kwa kupendwa barani Afrika."
        Mafunzo haya kwa makocha yatahusisha              mafunzo ya darasani kwa nadharia na uwanjani kwa vitendo.               Ikiwa ni sehemu ya mafunzo hayo, makocha hao watatoa baadhi              ya siri za mafanikio ya FC Barcelona ili kusaidia kuleta              utaalamu wa kimataifa kwenye soka la Tanzania.
        
Comments
Post a Comment