LUKE SHAW ASEMA HANA PRESHA KUZIBA NAFASI YA PATRICE EVRA



LUKE SHAW ASEMA HANA PRESHA KUZIBA NAFASI YA PATRICE EVRA
LUKE SHAW ASEMA HANA PRESHA KUZIBA NAFASI YA PATRICE            EVRA

BEKI mpya wa Manchester United Luke Shaw amesema hana mashaka yoyote ya kuziba pengo la mkongwe aliyetimkia Juventus, Patrice Evra.

Luke Shaw mwenye umri wa miaka 19 amesajiliwa na United kiangazi hiki kutoka Southampton kwa ada ya pauni milioni 27.

Beki huyo kinda wa kimataifa wa England ambaye alikutana na Evra hoteli huko Baverly Hills wakati beki huyo wa Ufaransa alipokwenda kuwatembelea wachezaji wenzake wa zamani, amesema yuko tayari kwa changamoto ya kuzipa pengo la Evra.

"Sijisikii kuwa na shinikizo lolote kuvaa kiatu cha Evra," alisema Shaw. Amekuwa mchezaji muhimu kwa United kwa miaka 10, natumaini nitaendeleza makali yake.

"Najua siku zote kutakuwa na shinikizo, lakini nitazingatia na kujali mchezo wangu uwanjani.

"Ukiwa chini ya kocha mpya, unahitaji kuonyosha uwezo wako mazoezini na hicho ndicho ninachokifanya.

"United ni timu kubwa duniani na hilo ndilo linalonisukuma kuonyesha ubora wangu ili kuthibitisha kuwa nina uwezo wa kuitumikia timu bora duniani."



Comments