LIVERPOOL imaifunga              kwa penalti 3-1 Manchester City kufuatia sare ya 2-2 ndani              ya dakika 90 katika mchezo wa Kombe la Kimataifa kujiandaa              na msimu mpya Uwanja wa Yankee, Marekani. 
        Man City ilipata              mabao yake kupitia kwa Stevan Jovetic dakika za 53 na 67              wakati mabao ya Liverpool yalifungwa na kwa Jordan Henderson              dakika ya 59 na Raheem Sterling dakika ya 85.
        Mikwaju ya penalti ya              Yaya Toure na Jesus Navas iliokolewa na Mignolet wakati pia              Aleksandar Kolarov naye alikosa kwa kupaisha- hivyo kumpa              nafasi Lucas Leiva kuipa ushindi wa 3-1 timu ya Brendan              Rodgers. Iheanacho pekee aliifungia City. 
        Sturridge pia              alipaisha penalti yake, lakini Emre Can na Henderson              walifunga kabla ya Lucas kutumbukiza kambani ya ushindi.
        Timu hiyo ya              Merseysiders sasa itamenyana na AC Milan mjini Charlotte              Jumamosi ikiwa na nafasi ya kuongoza kundi lake- ili ikutane              na mahasimu, Manchester United inayofundishwa na Louis van              Gaal mjini Miami.
                
Comments
Post a Comment