KOCHA HARRY REDKNAPP ASEMA LOIC REMY HANA TATIZO LA KIAFYA …adai Liverpool wana lao jambo




KOCHA HARRY REDKNAPP ASEMA LOIC REMY HANA TATIZO LA KIAFYA …adai Liverpool wana lao jambo

Bargain: Harry Redknapp signed Remy from Marseille                  for £8million in January 2013

KOCHA wa Queens Park Rangers, Harry Redknapp amesisitiza kwamba upo uwezekano mkubwa kuwa Loic Remy hajafeli vipimo vya afya Liverpool na ambapo amedai kuna sababu nyingine zilizochangia kushindikana kwa usajili wake.

Mshambuliaji huyo wa QPR ilikuwa akamilishe usajili wake wa kwenda Liverpool Jumapili lakini klabu hiyo ikatangaza kuwa Loic Remy amefeli vipimo vya afya.

Redknapp anaamini haiwezekani kuwa kufeli vipimo vya afya ndiyo sababu ya Remy kushindwa kukamilisha usajili huo wa pauni milioni 8.5.

"Sioni ni vipi amefeli vipimo. Haileti maana," alisema bosi huyo wakati utambulisho wa usajili wa Rio Ferdinand siku ya Jumatatu.

"Alifanya vipimo hapa, Maseille na New Castle. Alifanya pia na timu ya taifa ya Ufaransa kabla ya kombe la dunia.

"Hakuwahi kuwa na tatizo na afya yake. Sioni kabisa uwepo wa tatizo la afya, kutakuwa na tatizo lingine, hili la afya haliwezekani kabisa.

"Hakuwahi kufeli vipimo vya afya hapo kabla. Hakukosa hata mchezo mmoja Newcaste (Alipoitumikia kwa mkopo wa msimu mmoja).

""Liverpool watakuwa tu wamebadili mawazo yao au wameamua kwenda mwelekeo mwingine, wasisingizie kufeli kwa vipimo vya afya."



Comments