KIVUMBI KWENYE NAFASI YA GOLIKIPA ARSENAL … kipa wa Colombia David Ospina akamilisha usajili, kugombea namba na Wojciech Szczesny


KIVUMBI KWENYE NAFASI YA GOLIKIPA ARSENAL … kipa wa Colombia David Ospina akamilisha usajili, kugombea namba na Wojciech Szczesny

Shop window: David Ospina helped Colombia reach the                  quarter-finals of the World Cup in Brazil

ARSENAL imekamilisha usajili wa kipa wa Nice David Ospina kwa ada ya pauni milioni 3.2, kocha wa timu hiyo ya Ufaransa Claude Puel amethibitisha.

David Ospina aliivutia Arsenal baada ya kuonyesha uwezo wa hali ya juu kwenye michuano ya kombe la dunia akiwa na kikosi cha Colombia na kuisaidia nchi yake kufika hatua ya robo fainali kabla ya kutolewa na wenyeji Brazil.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 anakwenda kuziba pengo la Lukasz Fabianski ambaye ametimkia Swansea.

Ospina atalazimika kupigania nafasi ya kuwa chaguo la kwanza dhidi ya kipa namba moja wa Arsenal Wojciech Szczesny ambaye sasa anaingia kwenye uwezekano wa kuporwa namba.

Kocha Arsene Wenger amesisitiza kuwa kiwango cha kila mmoja wao ndio kitakachoamua nani atakuwa kipa namba moja.

Jina kamili:       David Ospina Ramírez

Tarehe ya kuzaliwa:           31 August 1988 (miaka 25)

Mji aliozaliwa:Medellín, Colombia

Klabu alizozitumikia:

2008–2014           Nice- mechi 177

2005–2008          Atlético Nacional      - mechi 97

Timu za taifa:

2006–2007          Colombia chini ya miaka 20  - mechi 12

2007–          Colombia    timu ya wakubwa - mechi 44



Comments