NI kama vile kauli ya mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Chocky imetimia – madansa watatu waliotimuliwa Extra Bongo baada ya kushiriki onyesho la Twanga Pepeta lililojulikana kama Usiku wa Mwana Dar es Salaam, wamejiunga na Twanga Pepeta.
Habari za uhakika kutoka Aset zinasema madansa hao Danger Boy, Sabrina na Maria Soloma tayari wameanza mazoezi na Twanga Pepeta na watatambulishwa rasmi siku ya Idd Mosi.
Kabla ya kuhamia Extra Bongo, madansa wote hao watatu walikuwa watumishi wa Twanga Pepeta na hivyo ni kama wamerejea nyumbani.
Wakati wa kuelekea onyesho la Mwana Dar es Salaam, Chocky alisema onyesho hilo limelenga kudhohofisha bendi bendi pinzani kwa kupandikiza migogoro ya wasanii na wamiliki kupitia show hiyo.
Chocky akaongeza: "Ukitaka kuamni hilo subiri uone wanamuziki watakaotimuliwa kwa kushiriki onyesho hilo watajiunga na bendi gani, nina uhakika wote watachukuliwa na Twanga Pepeta. Wanataka kuwapata wasanii kirahisi kwa njia za panya".
Comments
Post a Comment