KAGASHEKI CUP 2014: HATUA YA ROBO FAINALI KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO KATIKA UWANJA WA KAITABA, MABINGWA WATETEZI BILELE FC KUANZA NA KAHORORO FC
Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu nane zilizosonga mbele kwenye hatua ya Robo Fainali KAGASHEKI CUP 2014 leo zinaanza kuonyeshana ubabe kati ya Mabingwa Watetezi Bilele Fc na Kahororo Fc kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini. Kwa ajili ya kuwania nafasi nne za kuingia hatua ya nusu fainali ya Ligi ya KAGASHEKI CUP Inayotarajiwa kuanza wiki ijayo. Timu ya Bakoba Fc ilipoteza na kutupwa nje kwenye Mashindano baada ya matokeo ya timu ya Kitendaguro kwenda vibaya katika hatua ya Makundi mtanange wa Mwisho. Timu zilizoleta changamoto na kuweza kussonga hatua hii ya Robo Fainali na ambazo si kawaida kupita hatua hii ni timu tatu ambazo ni Kagondo Fc, Kahororo na Timu ya Ijuganyondo ambayo mwaka Jana ilifanya vibaya katika mashindano haya ya Kagasheki ambayo mpaka sasa inachezwa kwa mwaka wa tano mfululizo sasa.
Timu nane zilizotinga hatua ya Robo Fainali ni Kashai, Miembeni, Kagondo, Ijuganyondo, Bilele, Kahororo, Rwamishenye na Kitendaguro.
Katika Hatua hii ya Robo Fainali hapatakuwa na dakika za nyongeza mchezo ukimalizika dakika 90 kwa sare ni Mikwaju ya penati na itakuwa mechi zinachezwa kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba kama kawaida.
Wachezaji wa Timu ya Kashai wakishangilia moja ya bao kwenye hatua ya makundi huku pia wakifurahia kusonga mbele hatua ya Robo fainali. Marafiki zao Bakoba Fc chalii!! wakitupwa nje!
Moja ya Patashika wachezaji wa timu ya Bilele wakifunika Mpira uliopigwa kona na kuufanyia kazi kwenye lango la wapinzania wao!!
Wachezaji wa Bilele Fc wakipata maelekezo kwenye moja ya mechi ya makundi hivi karibbuni
Mabingwa Watetezi Bilele Fc wakishangilia bao kwenye hatua ya makundi
Mashabiki Kaitaba
Moja ya Kivutio cha Fainali hizi ni Mashabiki uingia kwa Wingi kuona timu za Kata zao!
Wachezaji wa Kashai wakibanjuka tuu!!
Bilele Fc leo kuanza Robo fainali na timu ya Kahororo fc saa 10:00 jioni
RATIBA ROBO FAINALI - KAGASHEKI 2014
Timu nane zilizotinga hatua ya Robo Fainali ni
Kashai vs Miembeni kuchezwa kesho jumapili 27.07.2014
Kagondo vs Ijuganyondo ___
Bilele vs Kahororo kuchezwa leo jumamosi 26.07.2014
Rwamishenye vs Kitendaguro__
Comments
Post a Comment