JAHAZI HAPATOSHI DAR LIVE IDD MOSI …MASHAUZI CLASSIC HAPATOSHI MWANZA IDD MOSI


JAHAZI HAPATOSHI DAR LIVE IDD MOSI …MASHAUZI CLASSIC HAPATOSHI MWANZA IDD MOSI
JAHAZI HAPATOSHI DAR LIVE IDD MOSI …MASHAUZI CLASSIC            HAPATOSHI MWANZA IDD MOSI

WAKATI kundi la Jahazi Modern Taarab linatarajiwa kufanya onyesho kubwa la Idd Mosi kwenye ukumbi wa Dar Live Mbagala  jijini Dar es Salaam, Mashauzi Classic wao watafanya makamuzi kwenye mjengo unaokimbiza jijini Mwanza kwa sasa, Buzuruga Plaza.

Hakuna ubishi kuwa kwa sasa hivi Jahazi na Mashauzi ndio vikundi bora zaidi vya muziki wa taarab hivyo maonyesho haya mawili ndiyo yanayotarajiwa kuvuta zaidi hisia za mashabiki wa burudani.

Jahazi kama inavyotarajiwa itashusha mashambulizi yake nchini ya mwimbaji bora kiume wa taarab, Mfalme Mzee Yussuf huku Mashauzi Classic ikiwa na mwimbaji bora wa kike wa taarab Isha Mashauzi.

Wasanii wengine wa Jahazi wanaotegemewa kuitingisha Dar Live ni pamoja na waimbaji Prince Amigo, Leila Rashid, Hadija Yussuf, Mohamed Mtoto Pori na Fatma Mcharuko.

Kwa upande wa Mashauzi Classic, jiji la Mwanza litatemeshwa na waimbaji Hashim Said, Zubeida Malick, Abdumalick Shaaban, Thania Msomali na Asia Mzinga.

Ni wapi? Ni Dar Live ya Jahazi Modern Taarab na Buzuruga – Mwanza ya Mashauzi Classic Modern Taarab.



Comments