CHANZO MPEJA 
          IVORY Coast itatangaza jina la                  kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo kesho alhamisi                  mchana, kwa mujibu wa shirikisho la soka.
          Shirikisho lilisema kwamba,                  usaili wa mwisho kwa majina  matatu yaliyosalia                  unakamilika leo jumatano mjini Abidjaan, mji mkuu wa                  nchi hiyo na mji mkuu wa kibiashara.Mfaransa                  Herve Renard anaonekana kuwa ndiye atashinda nafasi                  hiyo, kwa mujibu wa vyanzo vya mtandao wa michezo wa Supersport.com ndani ya                  shirikisho la nchi hiyo.
          Beki huyo wa zamani mwenye                  miaka 45, aliyeiongoza Zambia kutwaa ubingwa wa kombe la                  mataifa ya Afrika, AFCON 2012, anafurahia kuungwa mkono                  na viongozi wakubwa wa soka na wizara ya michezo ya                  Ivory Coast.
          Hata hivyo, kocha wa zamani wa                  Sporting na Benfica, Jose Manuel De Jesus kutoka Ureno                  naye anaonekana kupewa nafasi ya juu kutokana na uzoefu                  wake mkubwa kwa soka la ulaya. Lakini hajawahi kuongoza                  timu ya taifa, kitendo ambacho vyanzo vinaeleza kuwa                  kitamuangusha katika nafasi hiyo.
          Herve Renard anapewa nafasi                  kubwa ya kuwa kocha mpya wa Ivory Coast
          Mfaransa mwingine, Frederic                  Antonetti, aliyeifundisha Rennes, pia anapewa nafasi                  miongoni mwa majina matatu ya mwisho yaliyotolewa wiki                  iliyopita na shirikisho la soka. Ingawa hana uzoefu wa                  kufundisha timu ya taifa, lakini ujuzi wake wa                  kuendeleza vipaji unampa nafasi ya kuchaguliwa.
          Zaidi ya makocha 37 waliomba                  kazi hiyo, akiwemo kocha wa zamani wa Tembo hao,                  Francois Zahoui. Katika orodha hiyo, majina yalipunguzwa                  mpaka matano na baada ya usaili wa pili yakabakia matatu                  ambayo yanasailiwa kwa mara ya mwisho.
          Kocha mpya atapewa kazi ya                  kuiandaa timu kwa ajili ya kufuzu kucheza michuano ya                  Afrika mwaka 2015 nchini Morocco.
        
Comments
Post a Comment