HAYA NDIO MATOKEO YA TUZO ZA AFRIMMA 2014 ALIZO KUWA ANAWANIA DIAMOND..!!! DIAMOND ANG'ARA ILE MBAYAA..!!!
Zinaitwa African Muzik Magazine              Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann              center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali              akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa              wanaowania tuzo.
        Good              news kwa mujibu wa meneja Babu Tale ni kwamba Diamond              ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki              na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni 'number              one rmx' alioufanya na Davido wa Nigeria.
        Kolabo              bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2              Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South              Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani              ft. Waganda Radio na Weasel 'kiboko changu' J Martins ft. Dj              Arafat 'touching body' na Rebees na Wizkid 'slow down'
        Tuzo              ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda              Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania,              Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na              Jackie Gosee wa Ethiopia.
        Lady              Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika              Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster              Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya              na Irene Ntale wa Uganda.
        Producer              bora wa mwaka tuzo yake imechukuliwa na Mtanzania Sheddy              Clever aliekua anashindana na Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa              Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash              Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.
        Tuzo ya Mtayarishaji bora              wa video imekwenda kwa Ogopa Dj's ambao ndio waliifanya ile              video ya kwanza ya 'My number 1′ ya Diamond Platnumz.
                  Screen Shot 2014-07-27                at 8.17.33 AM
        Tuzo              zenyewe zimetolewa kwenye hili jengo
        Stori              zaidi na pichaz vitafata baadae hivyo endelea kukaa karibu              na Baakubwamagazine.com ili ujue kilichotokea kwenye tukio              hili ambalo limewahusisha wakali wengine kama Davido, 2Face,              Fally Ipupa, Iyanya, Flavour, Wyre, Miriam Chemmoss na              wengine ambao ni sehemu ya watu kutoka nchi 17 za Afrika.
        
Comments
Post a Comment