EXTRA BONGO WANAKAMUA MWANZA IDD MOSI … MUUMIN NA DOUBLE SOUND WAKO KAHAMA …VIJANA JAZZ NDANI YA JET LUMO DSM

BENDI ya Extra Bongo inayoongozwa na Mzee wa Farasi Ally Chocky, leo Idd Mosi itafanya makamuzi yake katika ukumbi wa Jembe ni Jembe ulioko kwenye ufukwe wa ziwa Victoria jijini Mwanza.

Wakati Chocky na kundi lake wako Mwanza, swahiba wake Mwinjuma Muumin "Kocha wa Dunia" akiwa na bendi yake ya Doubl M Sound watakuwa na maonyesho mawili mjini Kahama.

Onyesho la kwanza litakuwa ni la mchana kwenye uwanja wa Halmashauri, wakati usiku watapatikana kwenye ukumbi wa JVC Pub.

Nayo bendi Vijana Jazz Air Pambamoto Saga Rhumba watafanya onyesho lao la Idd Mosi kwenye ukumbi wa Monie Junction ulioko Jet Lumo jijini Dar es Salaam.

Comments