EVERTON YAMCHUKUA JUMLA ROMELU LUKAKU …dili la pauni milioni 25, mkataba wa miaka mitano


EVERTON YAMCHUKUA JUMLA ROMELU LUKAKU …dili la pauni milioni 25, mkataba wa miaka mitano

True Blue: Belgium centre forward Lukaku spent last                  season on loan at Everton from Chelsea

ROMELU Lukaku yuko njiani kukamilisha usajili wake wa kutoka Chelsea kwenda Everton kwa dili la pauni milioni 25.

Mshambuliaji huyo alitarajiwa kujiunga na kikosi cha Jose Mourinho Jumatano mchana lakini mambo yamegeuka na sasa anaelekea England kukamilisha usajili wake Everton kwa mkataba wa miaka mitano utakaomwingizia pauni 75,000 kwa wiki.

Jumatano iliyopita, Lukaku aliyeitumikia Ubelgiji kwenye michuano ya kombe la dunia. Alitupia picha kwenye Twitter akiwa kwenye ndege mwingi wa tabasamu na kutupia maandishi: "Muda wa kuandika ukurasa mpya."

Nyota huyo wa miaka 21 alikuwa na maisha ya furaha pale alipoitumikia Everton kwa mkopo wa msimu mzima, akitupia wavuni mabao 15 katika mechi 31 za Ligi Kuu ya England.



Comments