EDINSON Cavani, wiki hii anategemewa kuweka msukumo ili aweze kujiunga na Manchester United.
Nyota huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka 27, amedhamiria kuwa na maongezi na timu yake ya PSG ili kujaribu kulazimisha usaji huo, linaadika gazeti la Sport Italia.
Cavani alisani mkataba wa miaka mitano PSG msimu uliopita na akaisadia kutwaa taji la Ligue 1.
Hata hivyo mshambuliaji huyo sasa anataka kutimka na tayari amemtaka wakala wake amtafutie timu Premier League.
Cavani alijiunga na PSG kwa pauni milioni 50 kutoka Palermo na United italazimika kulipa kiasi kama hicho ili kumpeleka nyota huyo Old Trafford.
Comments
Post a Comment