KUNDI kongwe zaidi la miondoko ya taarab, East African Melody halitapatikana jijini Dar es Salaam wakati wa sikukuu ya Eid el fitr na badala yake litakuwa Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko.
Kwa mujibu wa ratiba iliyowasilishwa Saluti5, siku ya Idd Mosi Melody watakuwa Kilwa Kivinje kwenye ukumbi wa Kivulini aka Jumba la Dhahabu. Idd Pili Melody watahanikiza raha zao kwa wakazi wa Kilwa Masoko ndani ya Welfare.
Nalo kundi la Super Shine Modern Taarab likiwa na mwimbaji wao mpya Issa Kamongo (pichani juu), siku ya Idd Mosi litakuwa mjini Bagamoyo kwenye tamasha kubwa la Idd litakalofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Sanaa.
Tamasha hilo litashirikisha pia muziki wa dansi, kizazi kipya pamoja na fani ya maigizo.
Comments
Post a Comment