EAST AFRICAN MELODY KULA IDD EL FITR KILWA …kurejea Dar Idd Tatu

EAST AFRICAN MELODY KULA IDD EL FITR KILWA …kurejea Dar Idd Tatu
EAST AFRICAN MELODY KULA IDD EL FITR KILWA …kurejea Dar            Idd Tatu

KUNDI kongwe zaidi la miondoko ya taarab, East African Melody halitapatikana jijini Dar es Salaam wakati wa sikukuu ya Eid el fitr na badala yake litakuwa Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko.

Kwa mujibu wa ratiba iliyowasilishwa Saluti5, siku ya Idd Mosi Melody watakuwa Kilwa Kivinje kwenye ukumbi wa Kivulini aka Jumba la Dhahabu. Idd Pili Melody watahanikiza raha zao kwa wakazi wa Kilwa Masoko ndani ya Welfare.

Melody watarejea jijini Dar es Salaam siku ya Idd Tatu ambapo usiku wake watajitoma ndani ya ukumbi wa Travertine kupiga onyesho maalum lililoandaliwa na Abbas Chezntemba "Cash Money". 

Comments