DROGBA AREJEA RASMI CHELSEA



DROGBA AREJEA RASMI CHELSEA

Mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga tena na Chelsea.
Drogba, 36, alishinda makombe 10 akiwa na Chelsea kuanzia mwaka 2004 hadi 2012, na alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka klabu ya Galatasaray ya Uturuki.
Meneja Jose Mourinho, mapema alisema Stamford Bridge ni kama "kwake" mchezaji huyo.
Drogba ameiambia tovuti ya Chelsea kuwa: "Ulikuwa uamuzi rahisi- sikuweza kukataa nafasi ya kufanya kazi tena na Jose."



Comments