DAR MODERN WANAZINDUA ALBAM MBILI TRAVERITNE IDD MOSI …WAKALI WAO YA THABIT IKO PUGU …G5 WAKO FLAMINGO MAGOMENI

KUNDI la Dar Modern Taarab leo linafanya onyesho kabambe la Idd Mosi katika ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni.

Katika onyesho hilo la aina yake, Dar Modern wanatarajiwa kuzindua albam mbili mpya kwa mpigo hii ikiwa ni miezi michache tu tangu wazindue albam zao nyingine mbili ndani ya ukumbi huo huo wa Travertine.

Nalo kundi la Wakali Wao Modern Taarab chini yake Thabit Abdul "Mkombozi"  (pichani juu) litafanya onyesho lake la Idd Mosi katika ukumbi wa Kilimahewa Pub huko Pugu Kigogo Fresh jijini Dar es Salaam.

Kundi la G5 Modern Taarab siku ya Idd Mosi litapatikana katika ukumbi wa Flamingo ulioko Magomeni Mwembechai kona ya kwa Sheikh Yahaya, Dar es Salaam.

Comments