CLAUDIO RANIERI AMEVUNA ZAIDI YA PAUNDI MILIONI 10 IKIWA NI FIDIA YA KUFUKUZWA KAZI..NA SASA UGIRIKI WAMEMTEUA KUWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA
Changamoto                ya Ugiriki: Claudio Ranieri anatarajia kuiongoza nchi hiyo                katika fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016
          Na                Mpeja  Blog
           KOCHA                wa zamani wa Chelsea, Claudio Ranieri ameteuliwa kuwa                kocha mpya wa timu ya Taifa ya Ugiriki.Ranieri katika                miaka kumi iliyopita amevuna zaidi ya paundi milioni 10,                akilipwa kama fidia ya kufukuzwa kazi, lakini Ugiriki                umemteua kuwa kocha mkuu wa nchi hiyo.Ranieri amesaini                mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kulibadili soka la                nchi hiyo.Kocha huyo amefukuzwa mara tano (5) katika miaka                10 iliyopita na kuvuna fidia kubwa ya paundi milioni                10.Ilifukuzwa kazi na klabu za Chelsea, Valencia, Inter                Milan, Juventus na Monaco baada ya kuvurunda mno.Licha ya                kuwa na rekodi mbovu katika historia ya kushinda makombe,                kocha huyo mwenye miaka 62 bado anaendelea kupata kazi                nzuri zenye ulaji wa kutosha.Alilipwa paundi milioni 4                mwezi mei baada ya kufukuzwa kazi katika klabu                yaMonaco.Akiwa Chelsea alipewa jina la utani la                'Tinkerman` kutokana na mfumo wake wa kubadili kikosi mara                kwa mara.
        Mzee                wa kufukuzwa: Ranieri siku za karibuni amevunjiwa mkataba                na Monaco na kuvuna paundi milioni 4 kama fidia.
        Uzoefu wa kutosha:                Claudio Ranieri siku za nyuma aliziongoza klabu za Chelsea                na Juventus
        Alifukuzwa Chelsea mwaka              2004 na kocha huyo mwenye miaka 62 amevuna paundi milioni 10              kama fidia baada ya kufukuzwa katika klabu nne ndani ya              miaka 10.
        Wakati Ranieri anafukuzwa              na Roman Abramovich mwaka 2004, bado alikuwa na miaka mitatu              katika mkataba wake darajani ambapo angevuna paundi miliobi              2 kama malipo ya mshahara.
        Alishutumiwa kwa tabia yake              ya kubadili kikosi na alipewa jina la utani la 'Tinkerman,              lakini mwaka huo akiwa anafanya kazi, Chelsea alishika              nafasi ya pili na kufika nusu fainali ya UEFA.
        Mafanikio hayo hayakutosha              kwa Abramovich, ambaye alikuwa tayari kumlipa fidia kutokana              na kumfukuza kazi kwasabau aliona kama ameshindwa kutimiza              malengo.
        Chelsea ililipa fidia              iliyokaribia paundi milioni 1 na bosi huyo aliondoka kwenda              Valencia kurithi mikoba ya Rafa Benetiz aliyeteuliwa kuwa              kocha wa Liverpool.
        Katika miezi nane ya kazi              nchini Hispania, alianza kutafuta kazi baada ya kuvurunda              akiwa na Valencia.Viongozi walichukizwa sana na timu yao              kutolewa katika mashindano ya UEFA  dhidi ya Steaua              Bucharest na kuamua kumfukuza kazi na alitoka na mkwanja wa              kutosha.
        Inaaminika kuwa Ranieri              alivuna mzigo wa paundi milioni 4 baada kufukuzwa kazi, na              ilimchukua miaka miwili kutulia kabla ya kupata kazi mpya.
        Ranieri                (kushoto) alipewa jina la utani la 'Tinkerman'  akiwa                katika klabu ya Chelsea kutokana na tabia yake ya kubadili                kikosi mara kwa mara.
        
Comments
Post a Comment