Athuman Idd 'Chuji'                baada ya kuikosa Azam fc sasa anasaka nafasi ya kusajiliwa                JKT Ruvu
        Na Baraka Mpenja, Dar                es salaam
        WANANDINGA                waliotamba na klabu za Yanga, Simba na Azam fc wanafanya                majaribio chini ya kocha mkuu wa JKT Ruvu, Fredy Felix                Minziro kwa lengo la kutafuta nafasi ya kusajiliwa kwa                ajili ya msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania                bara.Meneja wa JKT Ruvu, Joel Frank                Cibaya ameiambia MPENJA BLOG jioni hii kuwa wachezaji                wanaofanya mazoezi kwa muda mrefu sasa ni Henry Joseph                Shindika, Haruna Ramadhani Shamte, Betram Mombeki na                Jackson Chove.Pia Cibaya alimtaja aliyekuwa                kiungo mahiri wa Yanga, Athuman Idd `Chuji` kuwa                anajitokeza mara kadhaa katika mazoezi hayo.
        Betram Mombeki kutoka                Simba sc anaendelea kujaribu bahati yake JKT Ruvu.
        "Wapo wachezaji                wanaofanya mazoezi hapa. Na kwa bahati nzuri TFF                wamesogeza ligi mbele imekuwa ni nafasi nzuri ya                kuwaangalia,"Alisema Cibaya.
        "Mwalimu kuna wachezaji                anawatazamia. Kama unavyojua ana uzoefu na wachezaji wa                timu kubwa. Hakuna watu wasumbufu kama wachezaji wa timu                kubwa hususani kutoka Simba na Yanga"
        " Kwasababu wale                hawaamini kama wapo JKT Ruvu au wako Mtibwa. Wanadhani                maisha ya Simba na Yanga ndio yapo JKT Ruvu, kwahiyo                wanapovikosa vitu walivyopata Simba wanakuwa wasumbufu                zaidi".
        Katika hatua nyingine,                Cibaya aliwataja wachezaji waliosajiliwa kwa maana ya raia                na askari kuelekea msimu mpya wa ligi kuu unaotarajia                kuanza kutimua vumbi septemba 30 mwaka huu.
        
Jabir Aziz (kushoto)                anafanya majaribio JKT Ruvu
        Wachezaji raia                waliosajiliwa na JKT Ruvu ni: Ambrose Morris (kutoka                Zanzibar), Mohamed Faki (Ashanti) na Benjamin Haule (Ruvu                Shooting).
        Wachezaji askari                (wanajeshi) waliosajiliwa ni: Madenge Ramadhani, Issa                Kanduru, Nafo Sanane na Nurdin Mohamed (wote kutoka JKT                Oljoro).
        Cibaya aliwataja                wachezaji wawili waliostaafu soka kuwa ni Hussein Bunu na                Sostenesi Manyasi.
        Aidha, aliwataja                wachezaji askari walioachwa na kupelekwa JKT Oljoro kwa                mkopo kuwa ni: Abdallah Bunu, Stanley Mkomola, Bakari                Kondo, kessy Mapande Paulo Ndamko.
        Cibaya aliongeza kuwa                wapo wachezaji raia walioachwa na klabu hiyo ambao ni:                Omary Kapilima, Kalage Mgunda, Jamal Machelanga, Emmanuel                Swita, Sadick Mecky, Omary Mtaka, Stanley Mkomola, Salum                Machaku na Chacha Marwa.
        Kuhusu maandalizi ya                msimu ujao, Cibaya alisema wanaendelea vizuri kupanga                majeshi yao ili kufanya vyema tofauti na msimu uliopita.
        "Sisi tunaendelea                vizuri na maandalizi, kama unakumbuka hapa katikati                tulikuwa na majaribio na kufanikisha kupata wachezaji                mbalimbali,"
        "Kwasasa tunaandaa timu                ya wakubwa na wadogo. Tumefanya hivyo kama miezi mitatu au                miwili na nusu. Tumepata wachezaji wadogo wazuri, kama                ulikuwa unafuatilia tumefika mpaka robo fainali ya                mashindano ya Rolling Stone". Alisema Cibaya.
        
Comments
Post a Comment