SHIRIKISHO la soka la Brazil CBF limemtangaza aliyekuwa mchezaji wa Brazil Dunga kuwa kocha wa timu ya taifa kwa mara ya pili.
Dunga aliyeiongoza Brazil kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1994 aliwahi pia kuwa kocha katika mwaka wa 2006 hadi 2011.
Dunga amechukua pahala pake Luiz Felipe Scolari, ambaye alijiuzulu kufuatia kimbunga cha mabao 7-1 ambayo timu hiyo ililazwa na Ujerumani katika hatua ya nusu fainali
Dunga mwenye umri wa miaka 50 naye alifutwa kazi baada ya selecao kubanduliwa nje ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 katika hatua ya robo fainali.
Comments
Post a Comment