Tatizo                likaanza: Seydou Keita (wa pili kushoto) aligoma kupokea                mkono wa Pepe (wa nne kushoto).
          MSIMU                bado haujaanza, lakini tayari dunia imeanza kuzungumzia                upinzani wa Real Madrid na Barcelona.Lakini wakati huu klabu ya Katalunya              haijahusika-kiukweli, hisia mbaya zimekuja katika mchezo wa              maandalizi ya kabla ya msimu baina ya Real Madrid na nyota              wa zamani wa Barca.Mchezaji wa              Roma, Seydou Keita aligoma kusalimiana na beki wa Ureno,              Pepe na kumrushia chupa ya maji kabla ya mechi hiyo ya              kirafiki kuanza.
                    Mchezaji mwenzake na Keita akijaribu kumuondoa                  kwenye eneo la tukio baada ya wachezaji wa Real Madrid                  kuanza kulalamika
          Bifu: Keita alimrushia chupa ya maji Pepe (juu                  kabisa kulia) na kumlowanisha.
          Acha hizo!: Pepe (wa pili kulia) avumilivu                  ulimshinda baada ya chupa ya maji kutua karibu yake na                  akarudi kulianzisha.
            Pia inasemekana Pepe alikuwa na mzozo na Keita                  wakati wa mechi, lakini hawakunaswa na kamera.
            Haya yalitokea katika ushindi wa bao 1-0 wa Roma                  dhidi ya mabingwa hao wa Ulaya, jumatano asubuhi katika                  mchezo wa kombe la kimataifa la Guinness mjini Dallas.
            Pepe na Keita walikuwa na bifu miaka ya nyuma                  kwenye mechi za El Clasico na walipokutana tena                  wameliendeleza.
          Wawili hao wana              historia: Keita alimtuhumu Pepe kuwa alimuita nyani kwenye              mechi ya El Clasico ya Supercopa mwaka 2011.
        Historia:                Keita na Pepe hawakuwa marafiki ambapo mchezaji huyo wa                zamani wa Barca alimtuhumu mwenzake kwa kumuonesha ubaguzi                wa rangi.
          Safari                hii baada ya Keita kugoma kumsalimia mpinzani wake kabla                ya mechi, walitenganishwa na wachezaji wenzao, ambapo Iker                Casillas na Xabi Alonso walikuwa wapatanishi wa amani.
        Hasira:                Keita bado anaonekana kuwa na hasira wakati ikiongea na                mchezaji wa Real Madrid, Isco baada ya tukio hilo.NA MPEJA                BLOG
        
Comments
Post a Comment