BI MWANAHAWA ALI ATAKUWA JUKWAA LIPI IDD MOSI? Aonekana kwenye matangazo matatu: Tabora, Dar Modern na G5




BI MWANAHAWA ALI ATAKUWA JUKWAA LIPI IDD MOSI? Aonekana kwenye matangazo matatu: Tabora, Dar Modern na G5
BI MWANAHAWA ALI ATAKUWA JUKWAA LIPI IDD MOSI? Aonekana            kwenye matangazo matatu: Tabora, Dar Modern na G5

BI Mwanahawa Ali, mmoja wa waimbaji mahiri kabisa wa taarab lakini mwenye historia iliyojaa utata katika kila bendi anayoipitia, huenda akazua utata mwingine kwenye maonyesho ya Idd el Fitr hususan Idd Mosi.

Mwimbaji huyo mkongwe ameonekana kwenye matangazo matatu tofati ya Idd Mosi, mawili ya Dar es Salaam na moja la Tabora.

Mwanahawa kwa sasa ni msanii wa Dar Modern Taarab ambapo anatarajiwa kuwepo kwenye onyesho lao litakalofanyika Travertine Hotel Magomeni siku ya Idd Mosi kama tangazo linavyojionyesha.

Lakini Mwanahawa anaonekana pia kwenye tangazo la G5 Modern Taarab linalonadi onyesho la Idd Mosi litakalofanyika Magomeni Mwembe Chai kwenye ukumbi wa Flamingo.

Kama vile hiyo haitoshi, Mwanahawa Ali anaonekana tena kwenye  tangazo la onyesho la Nani Zaidi kati yake na Khadija Kopa litakalofanyika Tabora mjini.

Promota wa onyesho la Tabora ameihakikishia Saluti5 (tena ushahidi wa maandishi) kuwa wasanii wote wa onyesho wa onyesho hilo wakiwemo pia Jokha Kassim, Omar Teggo na Mauwa Teggo wamesaini mkataba wa kushiriki show hiyo.

Je Mwanahawa Ali atapatikana kwenye onyesho lipi? Jibu litapatikana leo.

 
 
 
 

 

 

 

 



Comments