KATIKA hali ya kushangaza, Mwimbaji mkongwe hakuoneka kwenye uzinduzi wa albam mpya ya bendi yake Dar Modern Taarab na badala yake akaenda kushiriki onyesho lingine lililofanyika mjini Tabora siku ya Idd Mosi.
Dar Modern walikuwa wanazindua albam kwenye ukumbi wa Travertine jijini Dar es Salaam na ndani ya albam hiyo kuna wimbo uliombwa na Bi Mwanahawa lakini bado mwimbaji huyo mkongwe akaamua kulitosa onyesho hilo.
Onyesho alilokwenda kushiriki Bi Mwanahawa lilifanyika Bwalo la Maafisa wa Polisi huku likishirikisha wakali wengine kama Hadija Kopa, Omar Teggo, Jokha Kassim na Mauwa Teggo.
Comments
Post a Comment