LIVERPOOL iko ukingoni kukamilisha usajili wa beki kisiki Dejan Lovren kwa ada ya pauni milioni 20 ambayo itamfanya mchezaji huyo kutoka Southampton awe beki ghali zaidi katika historia ya Liverpool.
Brendan Rodgers amekuwa akihangaika kumsajili nyota huyo wa Croatia kwa kipindi chote cha dirisha hili la usajili.
Hata hivyo Southampton ambayo tayari ilishawauza kwa Liverpool Adam Lallana na Rickie Lambert, ilikuwa haipo tayari kumwachia beki huyo.
Lakini mambo sasa yamebadilika, Southampton imebana hatimaye imeachia. Imekaa mezani na Liverpool na sasa uhamisho wa Dejan Lovren umeelekea kibla.
Ununuzi wa Dejan Lovren utaifanya Liverpool iwe imetumia pauni milioni 80 kwa dirisha hili la kiangazi ambapo kiasi hicho kinategemewa kuongezeka wikiendi hii pale mshambuliaji Loic Remy atakapokamilisha usajili wake wa pauni milioni 8.5.
Liverpool imekataa kueleza wapi ilipofikia kuhusu usajili wa Lovren lakini inaaminika beki huyo anatarajiwa kukamilisha vipimo vya afya Jumamosi.
Orodha ya mabeki ghali waliotangulia Liverpool ni hii hapa:
Mamadou Sakho - £18million (kutoka PSG)
Glen Johnson - £18million (kutoka Portsmouth)
Tiago Ilroi - £8million (kutoka Sporting Lisbon)
Andrea Dossena - £8million (kutoka Udinese)
Martin Skrtel - £6million (kutoka Zenit)
Comments
Post a Comment