BAADA YA KUTUA RASMI CHELSEA, DROGBA ASEMA KAMWE ASINGETHUBUTU KUKATAA NAFASI YA KUFANYA KAZI TENA NA MOURINHO


BAADA YA KUTUA RASMI CHELSEA, DROGBA ASEMA KAMWE ASINGETHUBUTU KUKATAA NAFASI YA KUFANYA KAZI TENA NA MOURINHO

New boy: Drogba returns to Chelsea after two                    years away from west London

DIDIER Drogba amekamilisha usajili wake Chelsea na kusema kamwe asingethubutu kukataa nafasi ya kufanya kazi tena chini kocha Jose Mourinho.

 

Drogba mwenye umri wa miaka 36, amesaini mkataba wa kukipiga Stamford Bridge kwa miezi 12 hii ikiwa ni miaka miwili tangu atimkie Shanghai Shenhua ya China na baadae Galatasaray ya Uturuki.

Mshambuliaji huyo wa Ivory Coast alisajiliwa kwa mara ya kwanza na Jose Mourinho ndani ya Chelsea mwaka 2004 kwa pauni milioni 24.

Baada ya kupata nafasi ya kuungana tena na Mourinho kufutia 'kutengana' kwao kwa miaka saba, Drogba akasema: "Ni uamuzi rahisi – nisingeweza kukakataa nafasi ya kufanya kazi tena na Jose. Kila mtu anajua namna nilivyokuwa na uhusiano wa kipekee na klabu hii na siku zote ilinifanya nijisikie kama niko nyumbani.  

"Uchu wangu wa kushinda bado pale pale na sasa najipanga kuangalia namna ya kuisaidia timu. Nina furaha sana kwa ukurasa huu mpya wa maisha yangu ya soka".

Mourinho naye amemzungumzia Drogba kuwa bado ni mmoja wa washambuliaji bora katika ulimwengu wa soka.



Comments