KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone ameweka wazi kuwa angependa kupata saini ya mshambuliajia wa Mexico na Manchester United "Chicharito".
Hernandez amekuwa akihusishwa na kutimka United dirisha hili la usajili kufuatia msimu mbovu aliokuwa nao Old Trafford.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alianza mechi sita tu za Ligi Kuu msimu uliopita akiachwa nyuma na washambulijiaji Robin van Persie, Wayne Rooney na Danny Welbeck.
Simeone amesema Hernandez ni mchezaji wa hali ya juu na anayeweza kuwa muhimu kwenye timu yoyote ile.
"Tunazungumza na wakurugenzi wa michezo na kuwaeleza aina ya mchezaji tunayemtaka na baada ya hapo ni juu yao kumsajili.
"Kukiwa na Javier Hernandez pamoja na wachezaji wengine wazuri, lolote linawezekana. Hatufungi mlango hadi dirisha la usajili litakapofungwa.
Comments
Post a Comment