ARSENAL imefanikiwa kumsajili beki wa kulia wa Southampton Calum Chambers kwa ada ya pauni milioni 12.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 19 ameichezea Southampton mechi 23 tu za kikosI cha kwanza, lakini Arsenal inaamini anatosha kabisa kuwa moja ya nguzo muhimu kwao.
Washika bunduki hao tayari wamemsaini Mathieu Debuchy kutoka Newcastle kwa pauni milioni 10, lakini Arsene Wenger akahitaji beki mwingine wa kulia baada Bacary Sagna kujiunga na Manchester City - huku Carl Jenkinson akiwa njiani kuondoka Emirates.
Chambers ni zao lingine la academy ya Southampton na amekuwa mchezaji wa kudumu wa kikosi cha U19 cha England.
Hadi sasa hivi, Southampton tayari imeshawauza Rickie Lambert, Adam Lallana, Dejan Lovren na Luke Shaw.
Comments
Post a Comment