AKUDO IMPACT KUNGURUMA MSASANI BEACH CLUB KAWE IDD MOSI …Idd pili na Idd tatu wako Zanzibar

AKUDO IMPACT KUNGURUMA MSASANI BEACH CLUB KAWE IDD MOSI …Idd pili na Idd tatu wako Zanzibar
AKUDO IMPACT KUNGURUMA MSASANI BEACH CLUB KAWE IDD MOSI            …Idd pili na Idd tatu wako Zanzibar

VIJANA wa Masauti – Akudo Impact watafanya onyesho kubwa la kifamilia ndani ya ukumbi wao wa nyumbani Msasani Beach Club Kawe siku ya Idd Mosi.

Rais wa bendi hiyo, Tarsis Masela ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litakalojulikana kama "Eid Family Bonanza" litaanza saa 9 mchana hadi saa 7 za usiku.

Masela amesema mashabiki watakaofika Msasani Beach watapata fursa ya kuusikia na kushuhudia 'live' wimbo wao mpya kabisa unaokwenda kwa jina la "Akudo Wanaume".

Sakuti5 imeambiwa Idd Pili Akudo watakuwa Zanzibar katika ukumbi wa Cholo Disco Bar & Restaurant ulioko Nungwi huku Idd Tatu wakiendelea kufanya makamuzi yao huko huko Zanzibar lakini safari hii wakipiga katika ukumbi wa Gymkhana Club.

Comments