ADAM LALANA AUMIA GOTI, NJE WIKI SITA



PIGO LA KWANZA LIVERPOOL … ADAM LALANA AUMIA GOTI, NJE WIKI SITA

Shame: Lallana had been in line for his Liverpool                    debut on their US tour but he will now miss out

LIVERPOOL imepata pigo baada ya kiungo wake mpya Adam Lallana kuumia goti, maumivu ambayo yatamweka nje ya dimba kwa wiki sita.

Adam Lallana aliyesajiliwa hivi karibuni kwa pauni 23.6 kutoka Southampton, amepata bahati ya kufanya mazoezi na Liverpool kwa siku nne tu kabla ya kuumia goti hali itakayomfanya akose mwanzo wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England hususan katika mechi dhidi ya Southamton, Manchester City na Tottenham.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England anategemewa pia kukosa mechi ya kufuzu Euro 2016 dhidi ya Switzerland Septemba 8.



Comments