YANGA WAANZA KUNOA MAKALI COCO BEACH, MAXIMO ATARAJIWA KUWASILI KESHO



YANGA WAANZA KUNOA MAKALI COCO BEACH, MAXIMO ATARAJIWA KUWASILI KESHO

Jerryson Tegere baada ya kuongezewa mkataba na timu yake ya Yanga amewasili mazoezini leo. (Picha na ukurasa wa Facebook wa Yanga sc).
Nizar Khalfan (kushoto) alikuwepo katika mazoezi hayo .
Kazi na dawa, baada ya mazoezi, wachezaji wakaanza kupunga upepo
 Nizar Khalfan (kushoto) hana masihara, anatafuta pumzi kali ya msimu ujao.
Picha zote zimechukuliwa kutoka ukurasa wa Yanga kwenye mtandao wa Facebook .
MAKAMU bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam imeanza mazoezi ya kujiwinda na msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu na kombe la Kagame katika Fukwe za Coco Beach jijini Dar es salaam.
Mazoezi hayo yapo chini ya kocha wa makipa, Juma Pondamali `Mensah` wakati huu klabu ikimsubiri kocha mpya, Mbrazil, Marcio Maximo ambaye anatarajia kuwasili kesho kama mambo yatakwenda kama yalivyangwa.
Mazungumzo ya Maximo na Yanga sc yalisimamiwa na bosi mwenyewe, Yufus Manji, hivyo kwa asilimia nyingi, Mbrazil huyo mwenye heshima zaidi nchini Tanzania kutokana  na mafanikio aliyoyapata wakati akiifundisha Taifa stars atatu kukinoa kikosi hicho chenye masikani yake mtaa wa Jangwani kariokoo jijini Dar es salaam.
Wakati Yanga wakiendelea kumsubiri Maximo, tayari aliyekuwa kocha msaidizi, Charles Boniface Mkwasa ameshaondoka na kuelekea Uarabuni.
Mkwasa amepata kazi nchini Saudi Arabia na taarifa zilibainisha kuwa ameenda kuungana na aliyekuwa bosi wake Yanga, kocha mholanzi, Hans Van der Pluijm alitetimka kwa makubaliano baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita.
Yanga imeweza kuweka wazi majina ya awali ya baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu.
Msimu uliopita Yanga ilikuwa na kikosi cha wachezaji 30 kutoka timu ya Wakubwa na wachezaji watano (5) kutoka timu ya vijana  (U20) waliokuwa wamepandishwa kwa ajili kupata uzoefu na kuiongozea nguvu timu ya wakubwa katika michezo mbalimbali.
Hata hivyo kutokana na ripoti ya benchi la ufundi iliyowasilishwa mara baada ya ligi kumalizika, wachezaji 11 wameachwa katika usajili na tayari uongozi umemalizikana nao na kuwa huru kutafuta timu nyingine.
Wachezaji hao ni: David Luhende, Athuman Idd "Chuji",  Geroge Banda -U20, Yusuph Abdul -U20,  Rehani Kibingu -U20,  Hamisi Thabiti, Reliants Lusajo, Bakari Masoud - U20,  Shaban Kondo,  Abdalllah Mguhi "Messi" U-20 na Ibrahim Job .
Yanga  imewaongezea mikataba ya miaka miwili miwili wachezaji wake Jerryson John Tegete, Said Bahanuzi, Nadir Haroub 'Cannavaro', Ally Mustapha `Barthez`,  Mbuyu Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua,  Simon Msuva.


Comments