MWANARIADHA wa kike Alysia Montano (mwenye jezi ya pink) ameshiriki mbio za mita 800 huko nchini Marekani huku akiwa na ujauzito wa wiki 34 (zaidi ya miezi saba).
Bingwa huyo wa taifa mara tano, alimaliza mbio hizo za hatua ya kufuzu kwa kutumia dakia 2 na sekunde 32.23, hii ikiwa ni wiki saba tu kabla ya kuelekea kujifungua mtoto wake wa kwanza.
Licha ya kumaliza wa mwisho, bado nyota huyo wa zamani wa Chuo Kikuu cha California mwenye umri wa miaka 28, alishangiliwa na kupata heshima kubwa mara tu baada ya kumaliza mbio hizo.
Comments
Post a Comment