Akizungumza mara baada                ya kuwasili nchini jana wakitokea Ethiopia Kocha wa Timu                ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban                Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake                walioteuliwa katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima                Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia                yamewajengea uwezo mkubwa.
        Alisema  kuwa walipokuwa                nchi Ethiopia kwa mazoezi wamejifunza mbinu mbalimbali                kutokana na kuwa na program za kuwajengea uwezo wachezaji                wake na wako tayari kwa mashindano ya  Jumuiya ya                  Madola . 
        "Nimatumaini yangu                wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na wenzao waliokuwa                mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu                walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu                heshima kubwa kwani wamepikwa wakapikika". Alisema Kocha                huyo. 
        Aidha kocha huyo amesema                kuwa uwepo mazingira mazuri na vifaa bora vya mazoezi                kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa wanariadha                hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili                nchini Ethiopia. 
        Kwa upande wake mmoja wa                wanariadha ambaye amebahatika kuitwa kwenye kikosi                kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix                amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa                wanamichezo watakao iwakilisha nchi katika mashindano ya                Olympic kupitia mchezo wa riadha. 
        Alphonce amesema kuwa                atatumia ujuzi alioupata nchini Ethiopia walipokuwa                wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
         Jumla ya wanariadha 9                na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni                jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na kuendeleza                Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya                Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi                ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za                Uturuki, China na New Zealand 
                 Kocha wa wachezaji wa Riadha                  waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya                  mashindano ya  Jumuiya ya                  Madola  yanayotarajia kufanyika                  kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw.                  Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya                  wanamichezo hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa                  Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar                  es Salaam jana.
                 Kocha wa wachezaji wa Riadha                  waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya                  mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajia kufanyika                  kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw.                  Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya                  wadau wa mchezo wa Riadha waliojitokeza kuwapokea                  wachezaji wa mchezo huo mara baada ya kuwasili katika                  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere                  jijini Dar es Salaam jana.
                :                    Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia                    kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya  Jumuiya ya                    Madola  yanayotarajia kufanyika kuanzia 23,                    Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki                    (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wanamichezo                    hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa                    Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es                    Salaam jana. Picha na Frank Shija - MAELEZO
        


Comments
Post a Comment