UJERUMANI YAITUNGUA MAREKANI GOLI 1 KWA BILA KATIKA KOMBE LA DUNIA




UJERUMANI YAITUNGUA MAREKANI GOLI 1 KWA BILA KATIKA KOMBE LA DUNIA

Thomas Muller mfungaji bao la Ujerumani
Baada ya mvua kubwa iliyonyesha Recife na kusababisha mafuriko kutishia kuahirishwa kwa mechi baina ya Ujerumani na Marekani, hatimaye hali ya anga ilikuwa murwa kwa mechi hiyo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu haswa kwa Marekani ambao walikuwa wanahitaji sare ya aina yeyote na kuomba kuwa Black stars ya Ghana wanakunguwaa iliwao waweze kusonga mbele ktika kundi G.
Na baada ya mbivu na mbichi kubainika Ujerumani na Marekani zote zilijikatia tikiti ya kushiriki mechi za raundi ya pili licha ya Ujerumani kushinda mechi hiyo kwa bao moja bila ya jibu.
Bao la pekee lilifungwa na Thomas Muller 
Ujerumani na Marekani zafuzu kwa raundi ya pili
Mshambulizi huyo wa Bayern Munich aliifungia Ujerumani bao lake la 9 katika mechi sawa na hizo .
Fauka ya mvua kubwa iliyonyesha mapema taswira katika uwanja wa Arena Pernambuco ulioko Recife ilikuwa n ushindani mkubwa baina ya Marekani na Ujerumani.

Kufuatia matokeo hayo Marekani sasa watakwenda el Salvador ilikuchuana na Ubeljiji jumanne ijayo katika mechi yao ya kundi la pili huku Washindi wa kundi hilo Ujerumani wakiratibiwa kumaliza udhia dhidi ya mshindi wa pili katika kundi H yaani ( Algeria ama Urusi)


Comments