UHOLANZI WAITANDIKA MEXICO 2-1 NA KUFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA



UHOLANZI WAITANDIKA MEXICO 2-1 NA KUFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA
TIMU ya Taifa ya Uholanzi imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ngumu ya Mexico.
Mexico walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 48 kupitia kwa Giovani dos Santos.
Katika dakika ya 88 kikosi cha Van Gaal kilisawazisha bao hilo kupitia kwa Wesley Sneijder. 
Na katika dakika za nyongeza, Klaas-Jan Huntelaar aliifungia Uholanzi bao la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penati.


Comments