Na Othman Khamis Ame, OMPR
Timu ya Soka ya African Boys ya Kijiji cha Kitope imetawazwa ubingwa wa mashindao ya Kombe la Zaweda baada ya kuitandika timu ya New Star ya Kiwengwa kwa Magoli 4 -3 katika pambano la fainal ya mashindano hayo yaliyoshirikisha Timu 12 za Soka za Jimbo la Kitope.
African Boys ya Kitope ilibeba kombe hilo la Zaweda baada ya kutoka suluhu ya bila kwa bila na wapinzani wake New Star ya kiwengwa kwenye dakika 90 za mchezo huo na kulazimika kupigiana Penalti zilizoibua mshindi wa pambano hilo lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Santiago Benabao uliopo Kitope.
Mgeni rasmi wa Fainali hiyo Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza African Boys ya Kitope ambayo ilipata fedha taslim shilingi Laki 500,000/-, Seti ya Jezi, Kikombe, Mipira pamoja na Seti ya Tv na Dikoda yake iliyotolewa na Mke wa Mbunge wa Jimbo hilo Mama Asha Suleiman Iddi.
Mshindi wa Pili New Star ya Kiwengwa ikazawadiwa shilingi Laki 300,000/- taslim, Jezi, Kikombe pamoja na Mipira wakati mshindi wa tatu Timu iliyoalikwa ya soka ya Mahonda Kids akajinyakulia shilingi Laki 200,000/- Taslim, jezi pamoja na mpira. Mapema Balozi Seif alikabidhi zawadi ya fedha taslim kwa washindi wa mashindano ya mchezo wa pete { netball } ambapo mshindi wa kwanza ni timu ya wanawake ya Biasha Kitope, mshindi wa Pili alikuwa timu mualikwa Mahonda na wa Tatu alikuwa Timu ya Mabanati wa Kitope " B ".
Akizungumza na wana michezo hao wa mashindano ya Zaweda Cup Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif alielezea furaha yake kutokana na zoezi zima la mashindano hayo lililoonyesha nidhamu ya hali ya juu na kuwataka wanamichezo hao kuhakikisha kwamba nidhamu hiyo wanaichukulia kuwa kigezo cha kuiendeleza katika michezo mengine itakayowakabili hapo baadaye.
Mbunge wa Kitope Balozi Seif ali Iddi akizungumza na wanamichezo mara baada ya kumalizika kwa fainali ya mashindano ya Zaweda Cup hapo uwanja wa michezo wa Kitope Wilaya ya Kaskazini " B". Kushoto yake ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini " B " Ndugu Hilika Khamis Fadhil.
Balozi Seif akikabidhi zawadi za mipira na jezi kwa timu shiriki za mashindano ya Zaweda Cup yaliyofanyika ndani ya Jimbo lake la Kitope.
Balozi Seif akikabidhi zawadi za mipira na jezi kwa timu shiriki za mashindano ya Zaweda Cup yaliyofanyika ndani ya Jimbo lake la Kitope.
Balozi Seif akikabidhi zawadi za mipira na jezi kwa timu shiriki za mashindano ya Zaweda Cup yaliyofanyika ndani ya Jimbo lake la Kitope.
Mabingwa wapya wa kombe la Zaweda African Boys ya Kitope wakishangilia ushindi wao dhidi ya New Star ya Kiwengwa kwa mikwaju ya Penalti 4-3 baada ya kumaliza muda wa dakika 90 bila kwa bila.
Wanandinga wa African Boys ya Kitope wakiitia mikononi seti ya TV aina ya Phillips na King'amuzi chake ikiwa ni miongoni mwa mzawadi walizojikusanyia baada ya kushinda fainali ya kombe la Zaweda dhidi ya New Star ya Kiwengwa. Picha na Hassan Issa wa OMPR
Comments
Post a Comment