Tabarez kujiuzulu kufuatia                      adhabu kali dhidi ya Suarez
                  Kocha wa Uruguay Oscar Tabarez amesema kuwa                  atajiuzulu kama mwakilishi wa FIFA katika kamati mbili                  tofauti za kiufundi kupinga adhabu kali iliyotolewa na                  shirikisho hilo dhidi ya nyota wa Uruguay Luiz Suarez.
                Tabarez                  anasema kuwa adhabu hiyo kali iliyotolewa ya marufuku ya                  miezi minne dhidi yake ilikuwa kisingizio tu FIFA                  inanjama dhidi ya Uruaguay .Tabarez, alidai kuwa FIFA                  ilitoa adhabu hiyo kufuatia ushawishi wa vyombo vya                  habari haswa za kizungu .Kocha huyo mwenye umri wa miaka                  67 anahudumu katika kamati mbili za kiufundi za FIFA.
              Tabarez alikuwa akizungumza kabla ya mechi ya              mkondo wa pili kati ya Uruguay na na Colombia itakayochezwa              jumamosi .
        Suarez alimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio              Chiellini Uruguay ilipowalaza mabingwa hao wa zamani wa              dunia 1-0 jumanne iliyopita.
        FIFA imeamuru asishiriki mechi yeyote ile kwa              kipindi cha miezi minne mbali na kulipa faini ya pauni              65000. (£65,680).
        Awali katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke alimtaka              Suarez atafute matibabu ya kisaikolojia wakati akitumikia              marufuku hiyo.
                    Valcke;                  Suarez anahitaji matibabu
              Hii si mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez              kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani wake ,              msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya              kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav              Ivanovic Aprili 2013.
        Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alirejea kwa              kishindo na akaifungia Liverpool mabao 31 na kuisaidia              kumaliza katika nafasi ya pili.
        Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka              wa 2013-2014 .
        Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe              vifijo na nderemo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa              Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka Brazil.
        
Comments
Post a Comment