Refa wa Kombe la Dunia aliyeingia matatani kwa kuonekana akishangilia ushindi wa Nigeria.





Refa wa kombe la dunia aliyeingia matatani kwa kuonekana akishangilia ushindi wa Nigeria.
Shola
Ombi la kutaka refa Peter O'Leary kuondolewa katika listi ya kuchezesha mechi kwenye michuano ya Kombe la dunia limepata sahihi elfu 20 kutoka kwa mashabiki wa Bosnia kutokana na kitendo alichofanya wakati wa ushindi wa timu ya Nigeria wa goli 1-0.

Hatua hiyo imetokana na picha iliyomuonyesha refa huyo akishangilia ushindi na kumkumbatia golikipa wa timu ya Nigeria Vincent Enyeama.
Mbali na kutaka refa huyo aondolewe kutoka kwenye michuano hiyo, pia mashabiki wanataka matokeo ya mchezo huo kubadilishwa na kuwa 1-1 kumaanisha bado timu yao ipo  katika mashindano.


Comments