Nike yaongoza mtanange wa makampuni ya vifaa vya michezo katika kombe la dunia Brazil



Nike yaongoza mtanange wa makampuni ya vifaa vya michezo katika kombe la dunia Brazil
 Na Sultani Kipingo 
wa Globu ya Jamii

Uwezo wa kifedha wa Nike unaipaisha kampuni hiyo katika vita vya Kombe la Dunia 2014 kwa kuiongoza kampuni ya Adidas kwa mabao 4 katika awamu ya makundi ya michuano hiyo huko Brazil. 
Kampuni ya Nike ambayo ndio kubwa zaidi duniani kwa vifaa vya michezo imeonesha umwamba wake baada ya nyota inayowadhamini kufunga mabao 61 katika awamu hiyo ya makundi, huku Adidas ikifuatia kwa magoli 57.
 Lakini Adidas wanaweza kupata ahueni kwa kuwa na njumu bora, kwa mujibu wa wataalamu wa mambo hayo. Kiatu cha Adizero kinachovaliwa na nyota wakali kama  Lionel Messi, Robin van Persie, Arjen Robben, Karim Benzema na  Thomas Muller kimechangua magoli 38 katika awamu hiyo, huku kiatu cha Nike cha Superfly IV kinachovaliwa na
Alexis Sanchez  wa Chile na Xherdan Shaqiri wa Uswisi kimepiga mabao 21 hadi sasa (kabla mechi za mtoano kuanza). 
Adidas pia wanaongoza katika chati ya magoli ya kusaidia, kwa kuchangia mabao 65 katika awamu ya makundi, dhidi ya 54 ya Adidas, wakati kampuni ya Umbro ikijikongoja kupata goli, na hadi sasa ina goli moja la usaidizi kwa mchezaji Mauricio Pinilla aliyetoa pasi katika mchezo wa Chile dhidi ya Australia, ila kiatu chao hakijafunga bao hadi sasa. 
Wachezaji wanaovaa kiatu cha Puma wamefunga mabao manane, wakati kampuni ya Mizuno na Warrior kila mmoja akichangia mabao matatu. Kampuni ya Under Armour pia imemaliza awamu ya makundi bila kupata bao. 
 Nike wanaomdhamini Neymar wa Brazil wana mabao 61
  Cristiano Ronaldo wa Ureno anadhaminiwa na  Nike
  Robin van Persie wa Uholanzi anavaa kiatu cha  Adidas aina ya Adizero 
Adidas wanaomdhamini Lionel Mesii wa Argentina wana mabao 57


Comments