NI NANI ZAIDI DOUBLE M SOUND YA MUUMIN NA TWANGA PEPETA …wataumana jukwaa moja ndani ya Kahama Juni 26
BENDI ya Double M Sound chini ya Mwinjuma Muumin ambayo kwa sasa imeweka maskani yake mjini Kahama, itaumana jukwaa moja na Twanga Pepeta Alhamisi hii.
Muumin ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litafanyika Juni 26 ndani ya Chillers Club.
Double M Sound ambayo inaundwa na wacharaza magitaa Ally Akida na Yahaya Mkango ambao pamoja na Muumin, wamewahi kuitumikia Twanga kwa nyakati tofauti, inategemewa kutoa upinzani mkali katika onyesho hilo ambalo limebatizwa jina la Nani Zaidi.
Muumin ambaye ndiye mratibu wa onyesho hilo, amesema mpambano huo umekuwa gumzo Kahama hasa kwa namna kituo maarafu cha radio cha mjini hapo, Kahama FM kinavyolinadi onyesho hilo.
Katika awamu ya kwanza ya uhai wa bendi ya Double M Sound mwanzoni mwa miaka ya 2000, iliibuka kuwa mpinzani mkubwa wa Twanga Pepeta, jambo linalopelekea onyesho lao la Kahama kuwa na mvuto wa kipekee.
Comments
Post a Comment