MCHEZAJI MAARUFU WA GHANA AWASHANGAZA WOTE KOMBE LA DUNIA BRAZIL NJE YA UWANJA SOMA HABARI KAMILI LIVE!!




MCHEZAJI MAARUFU WA GHANA AWASHANGAZA WOTE KOMBE LA DUNIA BRAZIL NJE YA UWANJA SOMA HABARI KAMILI LIVE!!
Mcheza soka wa timu ya taifa ya Ghana, Sulley Muntari, ni maarufu sana kwa umahiri wake anapokuwa dimbani kama alivyo maarufu katika simulizi tamu za ukarimu, upendo na kuwahurumia watu. Wakati michuano ya Kombe la Dunia ikiendelea Muntari ameonekana peke yake akizunguka katika mitaa ya Rio de Janeiro na kuwapa pesa watu maskini wanaoishi jirani na eneo ambalo timu yake inafanyia mazoezi katika jiji hilo.

Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu wa 2014 imeathiriwa na visa vya ubaguzi, mashabiki wakaidi na ukosefu wa usawa, lakini kiungo huyo wa Ghana Sulley Muntari anatengeneza vichwa vya habari tofauti kabisa kwa matendo haya ya wema na utu.

Mapema Alhamisi, siku mbili kabla ya mchezo ambao timu yake ilitoka sare ya 2-2 dhidi ya Ujerumani, Muntari aliomba ruhusa kutoka kwa Kocha wake Kwesi Appiah kwenda kutembea katika mitaa ya Trapiche (jirani na mji wa Maceio, ambapo timu yake imeweka makazi) na kuanza kutoa fedha kuwapa watu maskini katika eneo hilo. Ripoti moja inasema kuwa alikuwa akitoa kiasi cha R$350 (fedha ya Brazil), ambayo ni sawa na kiasi cha $160 kwa kila maskini aliyekutana nae.

Hatimaye polisi wa eneo hilo walimtaka aache kufanya hivyo.

"Siwezi kulisahau tukio hili," bwana Edivaldo aliyebahatika kupata msaada huo aliuambia mtandao wa Globo.com.
"Nimeishi katika jamii hii maskini nyuma ya uwanja wa soka wa Rei Pele kwa miaka arobaini lakini sikuwahi kuona kitu kama hiki. Hakuna hata siku moja mwanasoka alikuja hapa. Brazil haikunipa chochote lakini Muntari wa Ghana amenipa. Niwaunga mkono na kuwashangilia mpaka mwisho."
"Mimi na mama yangu mwenye umri wa miaka 80 tumepata R$350 [fedha za Brazil]," anasema Inês Corrêa, aliyekuwepo katika tukio hilo baada ya polisi wa eneo hilo kumzunguka Muntari. "Ninaamini alikuwa na R$5,000 lakini kwa bahati mbaya polisi walimzuia kufanya tendo hili jema. Katika eneo hili tunawaona wanasiasa pekee tena wakati wa uchaguzi."

Je, unajua kuwa wakati wa biashara ya Utumwa Waafrika zaidi ya milioni thelathini walipelekwa Brazil kupitia Bahari ya Atlantic katika matukio yanayojulikana kama Maafa? Ni dhahiri kuwa Muntari anajua kuwa wale wenye nyuso nyeusi nchini Brazil ni wenzetu. Zitazame mwenyewe nyuso za watu wa Brazil, kama wewe ni Mwafrika popote utakapokuwa hapa duniani basi wewe ni sehemu ya familia hii moja.

Suleyman Ali "Sulley" Muntari, aliyezaliwa Agosti 27 mwaka 1984, ni mcheza soka raia wa Ghana ambaye anacheza nafasi ya kiungo wa kati katika Klabu ya Milan ya Italia. Akiwa katika klabu yake ya Internazionale, aliisaidia kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa barani Ulaya kwa msimu wa mwaka 2009–10 na Ubingwa wa ligi ya nchini humo maarufu kama Serie A kwa mwaka 2008–09 na 2009–10. Pia alikuwa katika kikosi cha Portsmouth kilichoutwaa Kombe la chama cha Soka cha Uingereza, FA, kwa mwaka 2007–08. Ni kaka mkubwa wa mchezaji wa CFR Cluj Sulley Muniru.



Comments